Social Icons

Pages

Friday 29 August 2014

WATU 10 WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI HUKO MBEYA!

Watu kumi wakiwemo watoto wawili, wamefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari mawili.

Ajali hiyo imehusisha gari ndogo ya abiria maarufu daladala lenye namba za usajili T 237 BFB aina Toyota Hiace na gari kubwa aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 CSV.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo imetokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso ilikuwa ikiingia barabarani.

Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu hayajaweza kupatikana mara moja kutokana na kuwa katika hali mbaya ambapo Dereva wa Fuso akitokomea mara baada ya tukio.

R.I.P All na pole sana kwa familia

No comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates