Social Icons

Pages

Monday 8 September 2014

Okwi huru kucheza Simba

Utata wa Emmanuel Okwi umemalizwa rasmi na mchezaji huyo wa Uganda sasa yupo huru.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilikutana jana na kupitia masuala mbalimbali ikiwamo mgogoro wa kimkataba kati ya klabu ya Yanga na mchezaji Emmanuel Okwi.
Mkataba huo ulipitiwa na kamati ikiwamo kumsikiliza mchezaji mwenyewe pamoja na upande wa Yanga na kuridhika kuwa mkataba kati ya pande hizo umevunjika.
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura alisema jana kuwa mkataba wa pande mbili haupo kwa sababu Yanga ilikiuka kipengele namba 8 kuhusu malipo ya ada ya usajili.
“Yanga ikiwa mwajiri, haikutekeleza kipengele hicho cha kimkataba hadi kufikia Juni 27 mwaka huu ilipoandika barua TFF kuomba mkataba huo uvunjwe. Kwa maana hiyo Okwi ni mchezaji huru, hivyo yuko huru kujiunga na timu yoyote,” alisema Wambura.

No comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates