Social Icons

Pages

Friday 22 August 2014

Aveva amrudisha kundini Dewji

Kassim Dewji

Rais mpya wa Simba, Evans Aveva ameteua wajumbe wa kuunda Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo.Wajumbe hao ni Mohamed Nassoro ‘Kigoma’, Musley Ruwei na Salim Abdallah ‘Try Again’.Pia Aveva amemteua Hans Pope kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili akisaidiwa na Kassim Dewji, huku wajumbe wakiwa Said Tully, Mulamu Nghambi na Rodney Chiduo.Kamati ya Mashindano itaongozwa na Kigoma akisaidiana na Geofrey Nyange, huku wajumbe wakiwa Mohamed Mlanzi ‘Meddy’, Hussein Simba na Idd Kajuna.

No comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates