Social Icons

Pages

Tuesday 19 August 2014

DKT JOEL BENDERA; UJIO WA RAIS KIKWETE MOROGORO


Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete anatarijia kufanya ziara na kufungua miradi zaidi ya 27 ya serikali mkoani Morogoro ikiwemo mradi wa ujenzi wa daraja la mto Kilombero pamoja na miradi ya kilimo.
  
Akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu ujio wa Rais kikwete Mkoani Morogoro  ,Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Joel Bendera amesema ziara ya Rais Kikwete itakuwa na manufaa makubwa kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuweka hamasa ya maendeleo ndani kutokana na ufunguzi wa Miradi pamoja na uwekaji wa mawe ya msingi katika miradi ambayo bado haijakamilika.

Ziara hiyo ya Rais Kikwete inatarajiwa kuanzia wilayani Ulanga na kuhitimisha wilayani Gairo.
 
 Ujio wa Rais kikwete kwa wananchi wa Mkoa  wa Morogoro umesubiriwa kutokana na sababu za kutaka kumweleza matatizo ya migogoro ya wakulima na wafugaji.

No comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates