Social Icons

Pages

Monday 8 September 2014

MZOZO WA NIGERIA NA FIFA WAISHA

Mabingwa wa Afrika, Nigeria huenda wameepuka kufungiwa kimataifa kuhusiana na mzozo wa uongozi katika chama cha soka cha nchi hiyo. Mzozo huo sasa umesuluhishwa, baada ya Chris Giwa kuondoa madai kuwa yeye ndio rais wa shirikisho la sola la Nigeria NFF. Fifa iliipa Nigeria hadi Jumatatu kupata muafaka. Iwapo Nigeria ingefungiwa, ingekosa mechi ya kufuzu Kombe la Mataifa siku ya Jumatato nchini Afrika Kusini. Shirikisho la soka la Afrika, Caf lilisema wiki iliyopita kuwa Super Eagles wataondolewa katika michuano hiyo iwapo watashindwa kucheza maechi yao.

No comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates